Social Media

Sunday, 12 April 2020

HALI NA TABIA ZA MUNGU.


Neno "MUNGU" katika kiswahili lina maana ya "MUUMBAJI"; yaani muumbaji wa kila kinachoonekana na kisichoonekana, mbingu na nchi.
>Mungu ni UPENDO
*1 Yohana 4:7 Wapenzi, na mpendane; kwa kuwa pendo latoka kwa Mungu, na kila apendaye amezaliwa na Mungu, naye anamjua Mungu.
8 Yeye asiyependa, hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni upendo.
9 Katika hili pendo la Mungu lilionekana kwetu, kwamba Mungu amemtuma Mwanawe pekee ulimwenguni, ili tupate uzima kwa yeye.
(Yoh 3:16, Gal 2:20, Rum 5:7-8)
>Mungu ni MTAKATIFU
*Neno takatifu maana yake ni kitu, mtu au jambo lililo'tengwa'. Mungu ni mtakatifu kwa sababu;
Amejitenga na miungu ya uongo(sanamu), yeye ni Mungu pekee.(Isaya 1:4, 45:11,5,22)
Na pia kwa sababu amejitenga na dhambi.(Hab 1:12-13, 1 Yoh 1:5, Isa 59:1-2, Mk 10:18)
>Mungu ni BABA WA REHEMA na NEEMA
*Ni mambo mema na ya huruma apatayo mwanadamu kutoka kwa Mungu; mfano wokovu wa bure kwa kila aaminiye.(1 Kor 1:3, Zab 136:1-26, Efe 2:4)
>Mungu ana HASIRA na GHADHABU
*Ni kweli Mungu ni upendo pamoja rehema; walakini kwa watu waovu wasiotaka kutubu, yeye ni mwenye hasira.(Rum11:22, 2:4-11, Isaya 13:9-11, Ebr 10:28-31)
>Mungu yupo kila Mahali
Zab 139:7-12, 23:4, Yer 23:23-24, Mith 15:3
Je! Unafahamu hali na tabia nyingine za Mungu? Karibu tushirikishe!

About Admin

we are certified themeforest Developers, Google blogspot developer and UI designers. We are popular at JavaScript engineers. We are team of professinal programmers, developers work together and make unique blogger templates.

0 Comments:

Post a Comment

Copyright © All Rights Reserved ™

Designed by: Templatezy / Sb Game Hacker